Mauaji

Umoja wa Mataifa umetaka Mamlaka nchini Msumbiji kuchunguza ripoti kuwa wanamgambo wamewaua takribani watu 50 na kuwachinja wanawake na watoto katika Mji wa Carbo del Gado Kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa ya chombo hicho inasema kuwa Katibu Mkuu wa UN António Guterres “ameshtushwa“ na ripoti hizo.

Katika shambulio la hivi karibuni, wanamgambo wa Kiislamu waliubadili uwanja wa mpira wa miguu kuwa ‘’uwanja wa mauaji”, ambapo walikata vichwa na miili, ripoti zilieleza.

Matukio ya hivi karibuni ya kukata vichwa ni mfululizo wa mashambulizi yaliyotkelezwa na wanamgambo katika Mji ulio na utajiri wa gesi Cabo Delgado tangu mwaka 2017.

Watu 2,000 wameuawa na karibu 430,000 wameachwa bila makazi katika eneo hilo lenye mzozo linalokaliwa na idadi kubwa ya Waislamu.

Wanamgambo hao wanahusishwa na kundi la Islamic State(IS), ambao wanaonekana kuweka mizizi Kusini mwa Afrika.

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limewatuhumu wanajeshi wa Msumbiji kwa kufanya ukatili wakati wa kudhibiti vurugu hizo, lakini wizara ya ulinzi ilitupilia mbali ripoti hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *