Wananchi wa Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji, wameondokana na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama baada ya Shirika la Joy In the Harvest kuzindua kisima cha maji katika kanisa la MMPT Kibirizi.

Akizindua Kisima hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Esther Mahawe, amesema kuzinduliwa kwa kisima hicho kitasaidia wananchi wa kata ya kibirizi kwani wamekuwa wakitumia maji machafu ambayo yamekuwa yakisababisha mlipuko wa magonjwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Joy in The Harvest Mwenge Muyombi amesema kisima hicho hadi kinakamilika kimegharimu zaidi ya Milioni 32, huku akisisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha adhima ya kumtua ndoo mama kichwani inatimia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *