
Serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 84 kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kuchakata mawese katika kijiji cha Nyamhoza Halmashauri ya wilaya Kigoma Mkoani Kigoma.
Kaimu Mkurungezi wa Halmashauri hiyo Nasri Kirusha amesema kiwanda hicho kitakuwa chini ya Kikundi cha wajasiliamali wadogo cha Ilakoze kinachojihusisha na ukamuaji wa mawese katika kijiji hicho na kueleza kuwa kitaongeza thamani ya zao la mchikichi.
Naye afisa kilimo Halmashauri ya Wilaya Kigoma Bw. James Peter amesema ujenzi wa kiwanda cha mawese kitasaidia kuongeza uzalishaji wa mawese pamoja thamni katika soko la ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kigoma Bi. Esther Mahawe mara baada ya kutembelea eneo litakapojengwa kiwanda hicho ambalo litamilikiwa na kikundi cha akina mama wajasiliamali cha Ilakoze amesema kitarahisha utendaji kazi kwa wajasilamali hao.
Baadhi ya wanakikundi cha ilakoze na wananchi wa kijiji cha nyamhoza wamesema ujio wa kiwanda hicho kitawasaidia kukuza kipato kupitia shughuli za uchakataji wa mawese.