Capture

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amemuagiza Meneja wa shirika la umeme (TANESCO) Mbeya kutokukata umeme siku za ibada ili kufanikisha ibada kufanyika ipasavyo.

Homera ametoa maagizo hayo baada ya viongozi wa dini kulalamikia tabia ya shirika la umeme TANESCO kukata umeme mara kwa mara na wakati mwingine viongozi hao kushindwa kuendesha ibada ipasavyo.

Pia Askofu wa kanisa la la Pentecost Assemblies of God Tanzania Thomas Kongoro ameomba serikali ishughulikie kero ya kukosekana kwa huduma ya maji kwa muda mrefu.

#BONYEZA HAPA KUSIKILIZA RADIO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *