Wanaume Mkoani Kigoma wameanza kujitokeza zaidi kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa, hali inayotajwa kuchangiwa na ongezeko la elimu kuhusu haki za binadamu na umuhimu wa kupinga ukatili katika jamii. Kwa muda mrefu, vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikihusishwa zaidi na wanawake na watoto, huku wanaume wengi wakibaki kimya wanapokumbana na vitendo hivyo kutokana…