Ushirikiano wa mashirika yasiyo ya serikali, wadau pamoja na serikali ndio nguzo muhimu ya kusaidia kukuza na kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi. Serikali Mkoani Kigoma imeyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kuboresha huduma, kuongeza ubunifu na kuungana na serikali katika kusukuma maendeleo kwa wananchi ili kufikia malengo ya dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.